Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 29 August 2017

Aina 3 ya miti yenye uwezo wakutoa ahueni kwa wenye kisukari


Kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili.

Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la sukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika haja ndogo ya muathirika pia.

Miongoni mwa sababu ambazo hupelekea ugonjwa huu ni pamoja na kuishi maisha ya anasa, watu wasiojishughulisha na kazi za kutumia nguvu au mazoezi na wale wanaopenda kutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa kuongezwa sukari.

Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kukojoa mara kwa mara, kuhisi njaa mara kwa mara, kuhisi kiu ya maji mara kwa mara, kupungua uzito wa mwili pamoja na kuchoka kwa mwili mara kwa mara.

Hata hivyo ni vyema ikatambulika kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuponya ugonjwa , ila ni kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kawaida na miongoni mwa tiba asili inayoweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari kuishi maisha ya kawaida ni pamoja na matumizi ya majani ya mlonge na mwembe.

Mtaalam  Abdallah Mandai kutoka Mandai Products Company anabainisha kuwa majani ya mwembe yanapokuwa machanga na kulowekwa ndani ya maji safi na salama kisha kukamua maji hayo na kunywa glasi ya maji hayo hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kisukari kurekebisha sukari yake ndani ya mwili, lakini pia majani hayo ya mwembe yanaweza kukaushwa kupitia kivuli kisha baada ya kukauka vizuri yasagwe yawe unga laini na utumie kijiko cha chai katika glasi ya maji mara tatu kwa siku.

Pia mzambarau huweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari hii ni mara baada ya kuzikausha na kuzisaga ili kupata unga laini, kisha tumia nusu kijiko cha chai cha unga wa zambarau katika glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chochote.


Mbali na hayo, Mtaalam Mandai anaeleza kwamba majani ya mlonge nayo ni moja ya msaada mzuri kwa wenye kisukari kwani husaidia kurekebisha sukari ndani ya mwili, hii ni kutokana na uwezo wa majani hayo kuwa na uwezo mzuri wa kurekebisha kongosho na kuifanya ifanye kazi yake vyema mwilini.

Kwa maelezo au ufafanuzi kuhusu miti hii ya aina tatu unaweza kuzungumza na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa ofisi zetu zinapatikana Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment