Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 August 2017

Aina 4 ya viungo vya jikoni vyenye kuondoa maumivu ya 'joint'

Tatizo la kuhisi maumivu ya viungo husani sehemu zile za maungio yaani joint ni miongoni mwa matatizo ambayo yamekuwa yakiwakumba watu mbalimbali hasa wazee.

Aidha, tatizo hili pia huweza kuchangiwa na shughuli za mhusika anazozifanya kila siku.

Leo napenda tufahamu hivi baadhi ya viungo ambavyo huweza kutumika katika kusaidia kutuliza tatizo hilo.

1. Kitunguu swaumu.
Ni miongoni mwa kiungo chenye uwezo mzuri wa kupunguza tatizo la maumivu ya viungo, ili kiungo hiki kikusaidie kwa tatizo hilo unaweza kusaga na kutumia rojorojo yake kuchua zile sehemu zenye maumivu na utaona matokeo mazuri ikiwa utafanya angalau kwa wiki nzima.

2. Tangawizi
Hiki ni kiungo ambacho kimekuwa kikitumika sana jikoni hususani kwa kuongeza ladha ya chai, lakini wengi wamekuwa hawafahamu kuwa matumizi ya kiungo hicho huweza kupunguza pia tatizo la maumivu ya viungo ndani ya mwili.Unachopaswa kufanya ni kusaga tangawizi kisha changanya kwenye maji y moto halafu kunywa kila siku asubuhi na jioni.

3. Mdalasini
Hii nayo hupunguza kiwango cha maumivu ndani ya mwili huweza kufanya vizuri pale inapochanganywa na kiwango kidogo cha asali ndani ya maji ya moto na kutumika asubuhi kabla ya kula chochote.

4. Manjano/ binzari
Ni kiungo kizuri pia kwa wenye shida ya maumivu ya viungo unachopaswa kufanya ni kuandaa vizuri kisha tumia mara moja kila siku.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment