Friday, 11 August 2017

Aina 5 ya vitamin ambazo huhitajika mwilini karibu kila siku

Binadam mwenye afya njema siku zote huhitaji virutubisho, vitamin na madini mbalimbali kutoka kwenye chakula anachokula kila siku.

Leo naomba nikwambie vitamin 5  muhimu ambazo binadamu ili awe na afya njema huhitaji karibu kila siku:-

1. Vitamin A
Hii ni muhimu kwa kuboresha uwezo wa kuona pamoja na kuimarisha kinga za mwili pia 

Miongoni mwa vyakula ambavyo huleta vitamin hii mwilini ni pamoja na samaki, mboga za majani, karoti n.k/

2. Vitamin E 
Hii ni vitamini muhimu kwa afya ya ngozi na nywele na vitamini hii hupatikana zaidi kwenye vyakula kama karanga, mboga za majani n.k

3. Vitamin B6
Hii ni muhimu kwa sababu husaidia kuboresha afya ya akili na kufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa mzuri zaidi.

Vitamin hii hupatikana kwenye maharage, mboga za majani, maziwa, mayai , samaki, viazi nk

4. Vitamin C 
Hii husaidia kuimarisha kinga za mwili na kuboresha afya ngozi pia 

Hii hupatikana nzaidi kwenye chungwa, limao n.k

5. Vitamin D
Hii ni muhimu kwani husaidia kwenye afya ya mifupa mwilini na kuuwezesha mwili kunyonya vyema madini ya calcium.

Hii hupatikana kupitia mionzi ya jua hasa ya asubuhi, na pia hupatikana kupitia mafuta ya samaki n.k

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

1 comment: