Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 30 August 2017

Aina ya vyakula vinavyoshauriwa kutoendekezwa na mabinti


Mabinti huhitaji mlo kamili na chakula cha kutosha wakati wa makuzi yao zaidi ya wanawake watu wazima.

Hii ni kwasababu katika kipindi hiki cha makuzi na kupevuka msichana huhitaji viini lishe vya kutosha kama vile protini, madini ya chuma na 'zinc' sambamba na vitamini, wanga na mafuta pia huhitajika kwa wingi.

Kwa kawaida wakati wa makuzi ya mabinti huweza kusababisha kupoteza damu wakati wa hedhi na mchakato wa kukua huongeza mahitaji ya madini chuma katika mwili wa msichana. Hivyo msichana atahitaji kula chakula chenye asili ya mimea, kula matunda na maji ya matunda (juice) kwa wingi.

Halikadhalika mabinti huhitaji kula nafaka na mboga za majani pamoja na vyakula vitokanavyo na mizizi kama karoti, viazi na vyakula vingine vyenye kuongeza nishati mwilini.

Vyakula vya kuepukwa na mabinti
Wasichana wanapaswa kuepuka vyakula visivyo na viini lishe vya kutosha, vyenye sukari nyingi, chumvi nyingi pamoja na mafuta mengi ambavyo huandaliwa au kufungashwa viwandani .

Vyakula vya namna hii, vinaweza kusababisha madhara kama vile uzito mkubwa, matatizo ya choo, shinikizo la damu, kisukari pamoja na magonjwa ya figo n.k

Pia wasichana wanapaswa kuepuka ulaji wa kiasi kikubwa cha nyama na mafuta na kuepuka vinywaji vyenye vilevi kama vile pombe.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa kwenye simu yako kutoka kwetu kila au kila mara tutakapokuwa tunapost.

No comments:

Post a Comment