Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 15 August 2017

Chanzo cha maumivu ya matiti & vyakula vya kupunguza maumivu hayo


Baadhi ya wanawake wamekuwa wakilalamika kwa kuhisi maumivu kwenye matiti na kushindwa kujua nini cha chanzo chake.


Kwanza ni vyema ikafahamika kuwa maumivu hayo huweza kutokea kwenye matiti yenyewe au pembeni yake.

Mwanamke mwenye tatizo hili huweza kuhisi maumivu pale anapoyashika matiti, jambo ambalo hupelekea wanawake kupata hofu zaidi, huku wengine wakihisi huenda ni dalili za saratani.

Aidha, maumivu hayo yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote, huku yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda.

Kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha maumivu ya matiti zikiwemo hizi  zifuatazo:

1. Kukoma kwa hedhi (menopause)
2. Hali ya mabadiliko ya vichocheo vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. hali hiyo huchangia matiti kujaa na kuuma na kusababisha mumivu hayo.
3. Maambukizi ya matiti
4. Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
5. Kutanuka kwa mirija ya maziwa
6. Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.

Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kwamba mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani, lakini vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo huweza kupunguza maumivu hayo.

1. Vyakula vyenye vitamin A, mfano karoti, spinachi, hoho n.k

2. Vyakula vyenye vitamin E, mfano, maboga (mbegu), samaki, karanga, parachichi n.k

3. Vyakula vyenye kiwango kidogo cha sodium. Mfano mboga mboga na matunda, 

4. Kunywa maji ya kutosha na juisi na kuepuka vinywaji kama bia, kahawa n.k

Kwa ushauri zaidi kuhusu vyakula na lishe unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaizt@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment