Tuesday, 8 August 2017

Faida 4 za vimiminika vya matunda (juisi) mwilini mwako

Mara nyingi tumekuwa tukieleza kuhusu faida za aina tofauti tofauti za juisi za matunda pamoja na juisi za mbogamboga.

Sasa leo siku ya nane nane nimeona ni vyema nieleze kwa ujumla wake kuhusu faida za juisi bila kujali ni juisi ya aina gani au matunda yapi.

1. Kwanza kabisa faida mojawapo ya juisi ni kuboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni, hii ni kwa sababu juisi huupa mwili urahisi wa kumeng'enya kutokana na ilivyoandaliwa.

2. Husaidia kuupatia mwili nguvu pia, kwa hiyo pale unapohisi kuchoka unaweza kupata glasi moja ya juisi na itakusaidia kuurejeshea mwili nguvu.

3. Huupatia mwili virutubisho kwa uzuri zaidi hasa inapokuwa juisi halisi kabisa yaani si ile ya viwandani.

4. Husaidia kuondoa sumu mwilini na kuna baadhi ya juisi pia husaidia kupunguza mwili kutokana na aina ya juisi na matakwa ya muhusika.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment