Monday, 7 August 2017

Fenesi tunda lisilosifika sana, lakini lina umuhimu wake mwilini


Mara nyingi ni nadra sana kusikia wataalam wa afya wakiwashauri wagonjwa kutumia tunda la fenesi.

Huenda kutokana na kuonekana ni tunda la watu wa aina fulani hasa wale wenye kipato cha chini, lakini ukweli ni kwamba tunda hili linafaida zake kiafya pamoja na kutopendekezwa sana na wataalam wa afya kama ilivyo kwa matunda mengine tuliyoyazoea.

Tunda la fenesi ni moja ya matunda ambayo mti wake ni mkubwa na wenye majani ya kijani kibichi. ndani ya tunda la fenesi huwa kuna mbegu .

Tunda hili hupatikana sana katika maeneo ya Asia na kwa hapa nchini unaweza kuyapata zaidi hata mkoani Morogoro.

Ndani ya fenesi kuna virutubisho kama vile vitamin A, C na B6 pamoja na madini ya potassium na calcium sambamba na madini ya chuma na magnesium.

Aidha, tunda hili ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo ni muhimu kwa upande wa umeng'enyaji wa chakula na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na shida ya kukosa choo mara kwa


Moja ya kazi ya fenesi ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili, lakini pia tunda hili huongeza vitamin C mwilini ambayo pia husaidia seli za damu kufanya kazi vizuri.

Kwa wale wenye shida ya upungufu wa damu yaani anemia tunda hili ni zuri pia kwao kutokana na kuwa na madini ya chuma 'iron' ambayo kwa kiasi kikubwa husaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini.

Ulaji wa fenesi pia husaidia kuongeza uoni mzuri kutokana na kuwa na vitamin A anbayo ni muhimu sana kwa afya ya macho, lakini pia fenesi husaidia kuimarisha afya ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya magnesium.

Kwa mengine mengi zaidi kuhusu fenesi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment