Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 5 August 2017

Hii ndio juisi yenye uwezo wa kufanya mambo 5 mwilini kwa mara moja

health benefits of apricot juice
Pindigesi ni matunda ambayo hupatikana katika sana mikoa ya Iringa kwa hapa Tanzania na ni miongoni mwa tunda ambalo huwafaa pia watu wenye kisukari.

Leo napenda kuzungumzia umuhimu wa juisi itokanayo na matunda hayo:-

1. Juisi yake ni nzuri kwa afya ya mifupa
Husaidia kuboresha afya ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya calcium, chuma , copper, magnesium na phosphor ambayo husaidia kuifanya mifupa kuwa imara mara dufu na kuzuia matatizo ya mifupa kuuma pia.

2. Huimarisha afya ya ngozi
Juisi hii ina kiwango kizuri cha vitamin C ambayo husaidia kuboresha afya ya ngozi, lakini pia husaidia kuimarisha afya ya nywele pia hasa katika nyanja ya ukuaji wake.

3. Juisi ya pindigezi ni nzuri kwa afya ya moyo
Juisi hii husaidia kuimarisha zaidi afya ya moyo  kutokana na kuwa na madini ya potassium yakutosha ambayo husaidia kuboresha afya ya mishipa ya damu mwilini.

4. Huzuia tatizo la kukosa choo
Si kila aina ya juisi huweza kusaidia kuondokana na tatizo hilo la kukosa choo lakini juisi hii huweza kusaidia tatizo hilo kutokana na kuwa na 'fiber' za kutosha ambazo husaidia kukinga na kuzuia tatizo hilo.

5. Ni nzuri kwa kinamama wajawazito.
Mara nyingi wakinamama wanapokuwa katika hali ya ujauzito hukumbwa na hali ya homa za asubuhi ambazo huitwa 'morning sickness' , hivyo wanapotumia juisi hii ya pindigesi huweza kuondoa hali hiyo.

Unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa ufafanuzi zaidi kupitia simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment