Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 26 August 2017

Je, ni kwa kiasi gani unatambua umuhimu wa mlo kamili kwa afya yako?

Siku zote afya ya mwanadamu hutegemea sana kinga alizonazo mwilini, kinga ambazo hujengwa kutokana na ulaji wa vyakula mbalimbali vyenye virutubisho kwa namna ambavyo Mungu ametujalia.


Kwa kawaida mwili unapaswa kujilindi wenyewe dhidi ya maradhi ya kila aina ukiwa na kinga imara, lakini pale inapobidi basi dawa ndipo huchukua nafasi yake katika kuusaidia mwili kupambana na magonjwa.

Kutokana na hayo yote inamaanisha kwamba mwili unahitaji mlo kamili ambao unajumuisha matunda, mboga za majani, nafaka na vyakula vingine vya asili, kwa sababu kila unachokula kina faida yake mwilini lakini siyo tu kula chochote kinachoitwa chakula bali ule chakula ambacho kitakuwa na maslai katika afya ya mwili wako.

Idadi kubwa ya watu wamekuwa hawapati chakula sahihi, badala yake wanakula vyakula ambavyo si tu ni hatari kwa afya zao, bali pia hudhoofisha kinga ya asili ya mwili na hivyo kuufanya mwili kubaki dhaifu na unaoweza kupatwa na magonjwa wakati wowote chanzo kikuu cha kushuka kwa kinga ya mwili kinasababishwa na ulaji wa vyakula visivyo sahihi ambavyo ndivyo vinavyopatikana kwa wingi kila mahali, hasa sehemu za mijini vyakula visivyofaa ndivyo vinavyotangazwa na kunadiwa kwenye vyombo vya habari kuwa bora. Hivyo kuna kila sababu ya kubadili mpangilio wako wa vyakula sasa ili ulinde afya yako.

Kwa ushauri zaidi kuhusu virtubisho asili kutoka kwetu unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa hivi karibuni kwa wewe mzanzibar tutakuwa karibu nawe pale Magomeni ambapo tunataraji kufungua tawi letu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment