Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 17 August 2017

Je, wanawake nao husumbuliwa na tatizo la nguvu za kike? majibu yapo hapa


Ni nadra sana kusikia watu wakizungumzia matatizo ya nguvu za kike, badala yake tumekuwa tukisikia matatizo ya kuhusu nguvu za kiume.

Mtaalam Abdallah Mandai anasema wanawake baadhi husumbuliwa na tatizo hilo kutohisi hamu ya tendo la ndoa au wanaposhiriki hupatwa maumivu kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kutoandaliwa ipasavyo hali hii ambayo huweza kutafsiriwa kama upungufu wa nguvu za kike kwa ujumla wake.

Lakini kutokana na tatizo hilo kuwa wazi zaidi kwa wanaume kwa maana ya maumbile yao, ni rahisi kujulikana huku wanawake wengi wakikabiliwa nalo bila yakutambua na hivyo kuwa kimya kimya zaidi.

Tatizo hili huwa ni gumu kujulikani kwa sababu si rahisi kumgundua mwanamke mwenye tatizo hilo na hii ni kwa sababu wanawake wengi wenye tatizo hili hujifanya kama hawana shida hii na pale wanapokuwa na mwanaume huonesha kwamba wanahisia ya kutaka kufanya tendo la ndoa huku uhalisia ukiwa ni tofauti.

Mara nyingi tatizo hili huweza kuchangiwa na homoni za mwanamke kutokuwa za kawaida au kuwa za juu zaidi ama chini.

Kiwango cha chini cha homoni huweza kuchangia mwanamke kukosa hisia za kufanya tendo, licha ya kwamba anaweza kuonekana kama hana tatizo hilo.

Hata hivyo, mtaalam huyo anaeleza kuwa ni vigumu wanawake kueleza matatizo yao ya kutojisikia hamu ya tendo la ndoa ukilinganisha na wanaume.

Pamoja na hayo, mtaalam wetu anashauri kuwa mwanamke mwenye tatizo hilo anaweza kutumia mboga za majani kwa wingi pia kupendelea kula tende.

Kwa mengine mengi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai moja kwa moja kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment