Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 14 August 2017

Juisi ya limao huwafaa wenye athma (pumu)

Pumu ni tatizo la kupumua ambalo mara nyingi huwapata watoto na hata watu wazima kutokana na hitilafu mbalimbali katika mfumo wa kupumua.

Pumu huweza kusababishwa na kuvimba kwa kingo za mirija ya kuvuta hewa, matatizo ya mzio (allergy), matatizo ya uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo pamoja na matatizo ya kisaikolojia.

Tatizo hili la pumu likishughulikiwa vizuri kwa watoto wadogo huweza kuisha kabisa.

Mara nyingi tiba ya pumu huwa hailengi katika kuponya kabisa bali husaidai kufifisha nguvu ya mashambulio ya pumu pale yanapotokea, pia kumbukuza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulio ya pumu kwa mgonjwa.

Moja ya njia inayoweza kutoa ahueni kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na hii ya kutumia tumia juisi ya limao.

Juisi ya limao inaaminika kuwafaa  watu wenye pumu kutokana na kuwa na kuwa na uwezo wa kuimarisha kinga za mwili na hivyo kusaidia seli kuharibika kirahisi ndani ya mwili.

Mgonjwa wa pumu anapokuwa na kinga imara huweza kuwa ni nadra sana  kushambuliwa na matatizo ya aina hii kwasababu mwili unakuwa na nafasi kubwa na nzuri ya kujilinda dhidi ya vitu mbalimbali kama vumbi, moshi wa sigara, manyoya ya wanyama n.k.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment