Friday, 11 August 2017

Makundi 3 ya vyakula yenye kuongeza madini muhimu mwilini


Kwa wale wafuatiliaji wa karibu wa mtandao huu naamini kwamba mtakumbuka kuwa tayari tumeshaelezana baadhi ya vitamin muhimu ambazo miili yetu huhitaji karibu kila siku.

Sasa leo ni zamu ya kufahamu baadhi ya madini ambayo huhitajika ndani ya mwili karibu kila siku.

1. Magnesium
Mwili huhitaji madini haya kwa ajili  ya kuboresha afya ya misuli, lakini pia husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.

Madini haya zaidi hupatikana kwenye vyakula aina ya nafaka, mboga za majani, matunda mfano ndizi n.k.

2. Calcium
Mwanadamu anapopata madini haya ya kutosha hasa mtoto husaidia ukuaji wake kuwa mzuri.

Pia madini hayo husaidia kuimarisha afya ya meno na mifupa  na pia huweza kutoa kuulinda mwili dhidi ya matatizo ya kisukari  pamoja na shinikizo la juu la damu.

3. Madini ya chuma (Iron)
Madini haya husaidia kukamirisha uzalishaji wa seli nyekundu za damu na hivyo mhusika kuepukana na tatizo la anemia (upungufu wa damu)

Madini haya hupatikana kwenye nyama, inaweza kuwa ya kuku au ng'ombe n.k

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment