Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 24 August 2017

Mbegu za uwatu & asali zinavyoweza kukusaidi kama unavidonda vya tumbo

Fenugreek Seed And Honey
Vidonda vya tumbo ni tatizo  linalotokea kutokana ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba kutengeneza kidonda/vidonda.

Ukuta wa tumbo huwa unatoa gastriki yenye mchanganyiko wa asidi ya haidrokloriki na vimenyenyo. Unapopata hamu ya kula au wakati unakula asidi hii huzalishwa na tumbo ili kumeng'enya chakula. Ukuta wa tumbo hufunikwa na layer ya 'mucus' ambayo huzuia asidi hii isitoboe ukuta wa tumbo au utumbo mdogo. 

Vidonda hivyo vya kwenye utumbo huweza kutokana na kutozingatia muda wa kula au maambukizi ya Helictobacter pylori, kuvuta sigara au matumizi holela ya dawa za kutuliza maumivu. asidi huzalishwa zaidi na hivyo kukwangua ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba na kusababisha vidonda kutokea.

Leo naomba nikueleza msomaji wangu mpendwa kuhusu mbegu za uwatu zinavyoweza kutoa ahueni kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo hasa mbegu hizo zikichanganywa na asali.

Unachotakiwa kufanya ni kupata mbegu hizo za uwatu kisha kiasi cha kijiko kimoja cha chakula kisha weka kwenye maji kiasi cha glasi moja yenye joto kiasi halafu ongeza asali kiasi cha nusu kijiko kidogo kisha tumia mchanganyiko huo kunywa asubuhi na jioni kwa mwezi moja asubuhi na jioni.

Kwa ufafanuzi zaidi au maelezo kuhusu lishe bora na asili au kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa hivi karibuni kwa wewe mzanzibar tutakuwa karibu nawe pale Magomeni ambapo tunataraji kufungua tawi letu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment