Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 17 August 2017

Mfulusana unaweza kukupatia faida hizi ukitumia mara nyingi


Duniani kuna matunda ya aina nyingi na kila tunda huwa na faida zake ndani ya miili yetu wanadamu.

Leo napenda tuangalie umuhimu wa tunda liitwalo blackberry au baadhi ya watu huweza kuyaita (mafulusana).

Matunda haya kwanza yanaladha nzuri lakini pia yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin A, C, E, K, B1, B2, B3, na vitamini B6.

Aidha, ndani ya matunda haya pia kuna madini mbalimbali ambayo nayo ni muhimu ndani ya miili yetu, madini hayo ni pamoja na madini ya chuma, 'calcium,' 'potassium', 'zinc' pamoja na magnesium.

Pia ndani ya matunda haya husaidia sana kuimarisha umeng'enyaji wa chakula ndani ya tumbo kutokana na kuwa na nyuzinyuzi na hivyo kupunguza uwezekano wa kukumbwa na tatizo la ukosefu wa choo.

Matunda haya pia huimarisha afya ya moyo kutoka na kuwa na madini ya 'magnesium' na nyuzinyuzi ambazo kwa pamoja husaidia kuzibua mishipa ya damu pale inapokuwa imeziba tatizo ambalo huweza kuchangia matatizo ya moyo.

Huimarisha kinga za mwili, matunda haya husaidia kuboresha kinga za mwili kutokana na kuwa na vitamini nyingi na madini kama zilivyoainishwa hapo juu.

Husaidia kulinda afya ya mifupa, Kama nilivyoainisha awali kuwa ndani ya matunda haya kuna madini yas calcium na magnisium ambayo huchangia kuimarisha mifupa.

Unaweza kutuuliza chochote kuhusu mimea tiba au nafaka au matunda nipigie kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment