Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 26 August 2017

Mwanamke: ukiona dalili hizi tambua kuwa si dalili nzuri kwako


Tunaposema uvimbe kwenye kizazi ni ile hali ya kuwa na uvimbe katika mfuko wa uzazi wa mwanamke ambao hujulikana kama 'fibroid'.


Uvimbe huo hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi. Tatizo hili huwakumba wanawake wengi hususani wale wenye umri miaka 20 hadi 30 yaani wale ambao wapo katika umri wa kuzaa.


Tatizo hili mara nyingi huwa halioneshi dalili za wazi linapokuwa katika hatua za awali, lakini baadaye huanza kuonesha dalili.

Miongoni mwa dalili za tatizo hili ni pamoja na kutokwa damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida.


Dalili nyingine ni kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpangilio maalum.

Pia mhusika wa tatizo hili huweze kuhisi maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, lakini pia huambatana na maumivu makali ya tumbo.

Hali ya uvimbe kwenye kizazi pia huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.


Dalili nyingi za tatizo hili ni mhusika kuwa na historia ya kutoshika ujauzito kwa muda mrefu au mimba kuharibika mara kwa mara.

Zingatia
Unapoona dalili hizo ni vyema ufanye maamuzi ya kuwaona wataalam wa masuala ya afya katika hospitali yoyote iliyokaribu nawe ili ufanyiwe uchunguzi zaidi na kuweza kupata msaada namna ya kuondokana na tatizo hilo.


Kwa ushauri zaidi kuhusu virutubisho asili vyenye uwezo wa kupambana na tatizo hilo unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa hivi karibuni kwa wewe mzanzibar tutakuwa karibu nawe pale Magomeni ambapo tunataraji kufungua tawi letu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment