Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 21 August 2017

Njia 3 maalum kwa wenye uhitaji wa kupunguza uzito

Baadhi ya watu wamekuwa wakipata tabu kutokana na kusumbuliwa na hali ya kuwa na uzito mkubwa na wasijue nini cha kufanya.

Wengi wamejikuta wakihangaika kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukaa bila kula pamoja na kufanya mazoezi.

Hapa leo napenda kukwambia baadhi ya hivi vyakula na vinywaji ambavyo huweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili.

1. Tangawizi
Tangawizi huweza kuunguza mafuta ndani ya mwili ambayo hutokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Unaweza kutengeneza tangawizi na kunywa kuanzia vikombe viwili hadi vitatu kila siku ili kupata matokeo mazuri zaidi.

2. Apple la kijani
Matunda haya yanauwezo mzuri wa kuunguza pia mafuta ndani ya mwili kutokana na kuwa na fiber pamoja na vitamin C yakutosha halikadhalika na kirutubisho kiitwacho antioxidants.

3. Broccoli
Hii ni miongoni mwa mbogamboga ambazo huweza kufanya vizuri katika kutatua tatizo la uzito mkubwa kwani huunguza mafuta ndani ya mwili.

Broccoli imesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin C, A, K ,B6, B12 pamoja na madini ya magnesium, folate pamoja na fiber ambazo virutubisho hivyo husaidia kuunguza mafuta ndani ya mwili na hivyo kupunguza uzito.

Unaweza kutumia kikombe kimoja cha juisi ya broccoli angalau mara 4 hadi 5 kila wiki.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment