Friday, 4 August 2017

Orodha ya vitu vitamu ambavyo baadaye hugeuka vichungu kwa afya yakoMagonjwa mbalimbali hususani yale yasiyoambukizwa mara nyingi husababishwa na namna tunavyoishi hususani katika masuala ya mlo. 

Siku za hivi karibuni magonjwa kama saratani mbalimbali, matatizo ya moyo, kisukari yamekuwa yakiwakumba watu wengi na hii ni kutokana na sababu ya vyakula vinavyosababisha magonjwa mbalimbali, na mbaya zaidi vyakula hivyo ndivyo huliwa zaidi kuliko vingine kutokana na kuwa na lladha nzuri mdomoni 

Leo tumeona ni vizuri tukuletee orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo vinaaminika kuwa na ladha nzuri lakini ni hatari kwa afya zetu.

Utumiaji wa vyakula vya kukaanga
Mara nyingi vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya, ikiwa ni pamoja na mhusika kuwa na uwezekano wa kuweza kupata saratani ya kwenye mfuko wa uzazi. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na chips na vingine ambavyo hupikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta. 

Matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi
Vyakula vyenye chumvi nyingi navyo huweza kusababisha saratani, kwani inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa saratani tumboni. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni kama vile vya kusindika, mfano nyama za makopo, maharage, n.k 

Kutumia sukari kupita kiasi. 
Matumizi mabaya ya sukari yamekuwa yakielezwa kusababisha saratani. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa katika vinywaji mbalimbali, mfano juisi soda, mara nyingi vinywaji hivyo huwa nasukari nyingi inayoweza kupelekea saratani ya kongosho. Sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula 

Unywaji wa pombe
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake na waume. Aina ya saratani zinazowezwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya ini, utumbo na koromeo. 

Matumizi ya nyama na mafuta
Watu wanaopenda kula nyama kila siku, huweza kuwa katika hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja na kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, uligundua kuwa watu wanaopenda kula nyama kila siku wako katika hatari ya kupatwa na saratani hiyo. 

Hivyo ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kukusababishia maradhi mbalimbali na hasa ya saratani, hivyo ni vizuri kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. 

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pamoja na hayo, bado unaweza kupakua Application yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment