Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 20 August 2017

Sababu 5 zinazokufanya mwanamke usihisi hamu ya tendo la ndoa

Tatizo la wanawake kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa ni miongoni mwa matatizo ambayo huwakumba baadhi ya wanawake ambao wapo katika ndoa na wale wa kwenye mahusiano.

Shida ni kwamba wanawake wengi wanatatizo hili na wameona kama ni hali ya kawaida kabisa, huku wasijue nini cha kufanya hivyo leo nimeona tujuzane hizi mbinu za kuweza kukusaidia kuondokana na hali hiyo.

1. Tatizo la kimahusiano kati ya mwaume na mwanamke.
Kwa kawaida ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga ndoa. Ikiwa uhusiano haupo vizuri ni rahisi ndoa hiyo kuingia katika matatizo. Mwanamke anaweza kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.


2. Matatizo ya kisaikolojia.
 Ikiwa mwanamke ana matatizo ya kisaikolojia ni rahisi kumfanya mwanamke akose hamu ya kushiriki tendo la ndoa, kwakuwa tendo la ndoa huwa ni hisia na huanzia akili na hivyo utulivu wa fikra ni muhimu ili mwanamke huyu aweze kulifurahia tendo la ndoa.


3. Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
Mwanamke mwenye matatizo ya kifedha au kikazi na yakamfanya afikiri sana juu ya matatizo hayo kuliko mambo mengine ya kimaendeleo ni rahisi mwanamke huyu kukumbwa na tatizo hili la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.


4. Manyanyaso ya kijinsia
Mwanamke mwenye historia ya kunyanyaswa kijinsia huathirika kisaikolojia. Mwanamke aliyebakwa au kukeketwa anaweza kakosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwani tayari akilini anakuwa anajeraha linalomfanya asione raha ya kushiriki katika tendo la ndoa.


5. Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
Ikiwa mwanamke akidharauliwa na akajua anadharauliwa na jamii ni rahisi kuathirika kisaikolojia na hivyo kupelekea kukumbwa na tatizo hili la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment