Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 29 August 2017

Tabia za kuziepuka ili ulale usingizi mnono


Punguza matumizi ya vinywaji vyenye kafeini, pombe na matumizi ya nicotini. Vitu hivi ni vichangamsho vya mwili na huathiri upatikanaji wa usingizi. Vinywaji vyenye kafeini ni vizuri vikitumika katika nyakati za asubuhi.

Ni vizuri kwa watu walio na umri mkubwa kupata muda wa kuota jua, au kufanya matembezi jua. Jaribu kupata angalau saa mbili ya mwanga wa jua kila siku. Fungua mapazia ya nyumba yako wakati wa mchana na jaribu kuota jua ndani kwako ukiwa umekaa kwenye kiti ukipendacho.

Jihusishe na shughuli mbalimbali za kijamii, za kifamilia na kazi mbalimbali ambazo zitakufanya usizubae na kuwa mchangamfu wakati wa mchana ambayo itapelekea kupata usingizi ulio mnono nyakati za usiku. Kama ni mstaafu jaribu kufanya kazi za kujitolea, kujiunga na makundi ya waliostaafu au kujiunga na elimu za watu wazima.

Hakikisha chumba chako kina utulivu, mwanga mdogo au giza na chenye joto linalohitajika (sio joto sana wala sio baridi sana) na kitanda chako ni chenye kufariji na katika hali ya usafi. Tumia chandarua katika chumba chenye wadudu wasumbuao na wasambazao magonjwa usiku, kwa mfano mbu.

Ondoa saa za ukutani katika chumba chako cha kulala kwa sababu mtu mwenye tatizo aangaliapo muda unavyosonga bila kupata usingizi, inaweza kumsababishia kuongeza tatizo la kukosa usingizi. Sauti na mwanga utolewao na saa za ukutani vyaweza kuwa visabishi vya kukosa usingizi pia.

Hakikisha kabla ya kulala, umekula chakula cha kujiridhisha, njaa wakati wa usiku yaweza kusababisha ukosefu wa usingizi. Zingatia kula mlo ambao ni mwepesi kabla ya kulala. Kula angalau saa tatu kabla ya kwenda kulala, Epuka kula chakula kingi na chenye viungo kwa wingi kwa kuwa inaweza kupelekea ugumu katika mmeng’enyo wa chakula nyakati za usiku na kukufanya kukosa raha na hata usingizi.

Fanya mazoezi mara kwa mara, kwa kuwa mazoezi yanasaidia kupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment