Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 19 August 2017

Vyakula 5 unavyoweza kula kama mbadala ya nyama nyekundu

 https://images.food52.com/GhBUthOnkbowQZpcze1nqKuEjnE=/753x502/d25d5d5e-51e0-4d18-8f23-259c7e4a5797--2016-1004_chicken-soup-with-coconut-milk-and-sweet-potatoes_bobbi-lin_355_1-.jpg
Habari za Jumamosi mdau wangu wa ww.dkmandai.com leo ni siku nyingine tena naomba nikukaribishe tuendelee kufahamishana mambo mengine mazuri kuhusu afya zetu.

Leo naomba tuzungumzie kuhusu mbadala wa vyakula unavyoweza kula badala ya kula nyama nyekundu ambazo huwa na madhara pale ambapo hutumika kupita kiasi, hivyo kwa kulitambua hilo nimekuwekea hapa chini orodha ya vyakula mbadala wa kitoweo hicho ambacho kwa kiasi kikubwa huongeza protini ndani ya mwili karibu tuvifahamu sote.

1. Viazi Mviringo
Viazi hivi  navyo huwa na protini hivyo pale unapokosa nyama unaweza kutumia viazi hivi kwa kuviandaa kama supu yake kisha unakula angalau kwa wiki mara mbili ili kujipatia protini ndani ya mwili wako.

2.Mayai
Mayai nayo ni mazuri kama chanzo cha protini lakini ni vyema ukapata mayai ya kienyeji kuliko yale ya kisasa ili kupata kiwango cha protini ya kutosha.

3. Uyoga
Mboga hii ya asili nayo inasifika kwa kuwa na kiwango kizuri cha protini hivyo huweza kutumika kama mbadala wa nyama na ikamsaidia mhusika kupata kiwango cha protini ndani ya mwili. Hata hivyo ni vyeama kuwapata wataalam wa uyoga kabla ya kuutumia kwani kuna baadhi yake huweza kuwa sumu.

4.  Maziwa
Maziwa ya n'gombe nayo ni chanzo kizuri cha protini  hivyo badala ya kutumia nyama kila siku unaweza pia kutumia maziwa na ukaendelea kuupatia mwili wako protini.

5. Karanga
Nazo zinakiwango cha protini hivyo huweza kutumika mara moja moja kama mbadala wa matumizi ya nyama nyekundu ambazo zikitumika kupita kiasi huweza kuwa na madhara.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment