Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 18 August 2017

Yafahamu maua haya ya mti ambayo huweza kusaidia matatizo yako pia


Mlonge ni mti ambao una asili ya India, lakini kwa sasa mti huu hupandwa kanda za tropiki kwa kifupi ni kwamba unapatikana maeneo mengi duniani

Karibu kila sehemu ya mti huu ni tiba yaani kuanzia mbegu zake, magome, majani, maua pamoja na mizizi. Sasa leo hapa mimi nitazungumzia kuhusu maua tuu!!
 
Maua ya mti wa mlonge nayo yana msaada wake katika matibabu na miongoni mwa faida za maua haya ni kumsaidia mama anayenyonyesha kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa.

Sambamba na hayo, maua ya mlonge pia husaidia kutoa ahueni kwa wenye matatizo ya haja ndogo (mkojo) kutoka kwa shida au ikiambatana na maumivu, kwahiyo matumizi ya maua huweza kuondosha tatizo hilo.

Maandalizi ya maua haya ya mlonge ili yatumike vizuri inabidi yachemshwe na kupata mfano wa chai iliyotokana na maua ya mlonge ambayo mhusika atahitajika kunywa chai hiyo kila siku kikombe kimoja asubuhi na jioni. kwa wiki mbili mfululizo

Hayo ndiyo machache ambayo nimeona nikwambie leo mdau wangu, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmanditz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment