Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Friday, 15 September 2017

Aina 3 za vinywaji vizuri kwa mamamjamzito

Mama mjamzito anapaswa kutazamwa kwa upekee sana wakati wote wa kipindi cha ujauzito ili kuweza kufahamu maendeleo na ukuaji wa ujauzito kwa ujumla

Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama mjamzito akiwa katika hali hiyo ni pamoja na ulaji na unywaji wa vinywaji mbalimbali.

Leo naomba nikuelezea hizi aina kadhaa za juisi ambazo hupendekezwa kwa mama mjamzito:-

1. Juisi ya karoti
Juisi hii humsaidia mama mjamzito kwenye upande wa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kumuepusha mama dhidi ya ukosefu wa choo kama ilivyo kwa wajawazito wengi.

Pia juisi hii husaiida kuboresha ngozi ya mama mjamzito kwani baadhi ya kinamama wakati wa ujauzito huharibika ngozi zao.


2. Juisi ya miwa
Kinywaji hiki ni chanzo kizuri cha vitami A, B1,B2, B3, B5,B6 na C pamoja na madini mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini ya antioxidants, protini na nyuzinyuzi ambavyo vyote ni muhimu kwa mama mjamzito.

3. Juisi ya Boga

Juisi hii husaidia kumuepusha mama dhidi ya kisukari cha mimba pamoja na ukosefu wa choo na kupunguza uwezekano wa shinikizo la juu la damu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment