Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 6 September 2017

Aina 5 ya vyakula ambavyo huimarisha mifupa yako

foods good for bones
Kuwa na mifupa imara ni moja ya mambo ambayo muhimu katika maisha ya kila mmoja wetu.

Lakini pia watoto na wanamichezo ni miongoni mwa makundi muhimu ambayo huhitajika kuwa na mifupa imara.


Leo naomba kukueleza kuhusu vyakula vyenye uwezo wa kuimarisha afya ya mifupa:-

1. Maziwa
Maziwa ni muhimu kwa afya ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya 'calcium', ambayo husaidi pia kuimarisha afya ya mifupa ya mwili.


2. Spinach

Mboga hii ya majani nayo husaidia kuongeza uimara wa mifupa ya mwili kutokana na kuchangia kiasi cha asilimia 25% ya madini ya calcium ndani ya mwili.

3.Mayai
Mayai yamesheheni vitamin D ambayo husaidia kuongeza uzito wa mifupa na kuipa uimara zaidi.


4. Ndizi
Tunda hili limesheheni madini ya calcium ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa

5. Samaki (salmon) 
Ndani yake huwa kuna virutubisho mbalimbali kama vile, omega 3, vitamin D, protini, calcium na fatty acid. Kwa pamoja kati ya vitamin D, omega 3 na fatty acid husaidia ongezeko la unyonywaji wa madini ya calcium ndani  ya mwili na hivyo kulinda afya ya mifupa.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment