Thursday, 28 September 2017

Chai ya maganda ya mkomamanga huponya mafindofindo (tonsil)


KOMAMANGA ni moja ya matunda yenye ladha nzuri ambayo hupatikana katika maeneo mbalimbali duniani.

Asili ya tunda hilo ni Iran pamoja na Kaskazini mwa India na hufahamika kama 'Punica Granatum' kwa jina la kisayansi. Pia tunda hili hupatikana katika mikoa kadhaa hapa nchini.

Tunda hilo hustawi kipindi cha mwezi Februari na Septemba na hustawi katika hali ya hewa ya joto. Mti wa mkomamanga pia umekuwa ukisifika kwa uwezo wake wa kuhimili hali ya hewa ya ukame.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii naamini utakumbuka kuwa ni mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu tunda hili, lakini leo nahitaji kukwambia faida za maganda yake.

Maganda ya komamanga yanasifika kwa kutatua matatizo kadhaa yakiafya kama ifuatavyo:-

1. Hulinda afya ya moyo
Kutokana na kuwa na antioxidants, ambayo husaidia kupunguza sumu za mwilini ikiwa ni pamoja na cholesterol. Hii ni kwasababu kama utakuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol huweza kuwa katika hatari zaidi ya kukumbwa na magonjwa ya moyo.

2. Inautajiri wa vitamin C
Vitamin hii ni muhimu kwa siha ya afya ya miili yetu kwa sababu huujengea mwili uhakika wa kuwa na kinga imara.

3. Huponya matatizo ya koo
Matumizi ya kinywaji kilichoandaliwa kwa kutumia maganda ya komamanga husaidia kuponya matatizo ya vidonda vya mdomoni na kooni ikiwa ni pamoja na mafindofindo (tonsil).

4. Huimarisha mfumo wa chakula
Chai itokanayo na maganda ya komamanga husaidia kuboresha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni 

Jinsi ya Kuandaa
Tafuta maganda ya komamanga na uyakaushe vizuri kisha usage na kupata unga mwepesi, kisha chemsha maji na uweke unga huo kwenye maji ya moto halafu funika mchanganyiko huo na kuuacha kwa dakika 25 kabla ya kunywa.

Baada ya dakika hizo unaweza kunywa kinywaji hicho kutwa mara mbili asubuhi na jioni kwa muda wa siku 5.

Kama utahitaji ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment