Monday, 18 September 2017

Dalili 5 ambazo hutakiwi kuzipuuza kwenye afya yako


Kuna baadhi ya vitu vinapotokea kwenye afya yako hupaswi kuvipuuza hata mara moja na badala yeke unatakiwa kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuwaona wataalam wa afya.

Leo ninazo hizi dalili kadhaa ambazo hupaswi kuzipuuza mara unapohisi au kuziona katika mwili wako.

1. Maumivu ya Kifua
Unapoona unahisi maumivu haya na huenda yanaambatana na kupata shida wakati wa kupumua ni vyema kuwaona wataalam kwani huweza kuwa dalili za matatizo ya moyo. Hivyo ni vyema kufanya uchunguzi zaidi ili kufahamu chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi mapema.

2. Damu kwenye haja ndogo
Hali hii mara nyingi huambatana na maumivu wakati wa kupata haja ndogo (mkojo) au maumivu ya mgongo na kiuno. Hali hii huweza kuwa dalili la shida ya mawe kwenye figo, lakini hali hiyo huweza kuwa dalili za maambukizi kwenye bofu cha mkojo. Hivyo ni vyema kuwaona wataalam kwa matibabu zaidi.

3. Shida kwenye upumuaji
Unapohisi zoezi la upumuaji kwako linakuwa ni chanagamoto tambua kuwa hilo si jambo nalo la kulipuuza na unapaswa kuwaona wataalam kwa uchunguzi zaidi kwani hali hiyo huweza kuwa ni dalili za matatizo ya mapafu, pumu na aina fulanifulani ya mzio.

4. Kuhisi kujiua
Unapohisi unazongwa na mawazo ya kuua au kujiua hiyo nayo si dalili njema kwako, hivyo unatakiwa kupata suluhisho la mapema kutoka kwa wataalam wa masuala ya saikolojia.

5. Kupungua kwa uzito kwa harakaTunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.No comments:

Post a Comment