Monday, 25 September 2017

Fahamu kuhusu mkaratusi unavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa


Mkaratusi ni kati ya miti inayopatikana  hapa nchini, sifa za mti huu mara nyingi huwa ni mrefu na huwa na majani membamba.

Mbali na sifa hizo pia mti huu umekuwa ukisifika kwa kuwa na uwezo wa kutatua changamoto kadhaa za matatizo ya kiafya.

Miongoni mwa matatizo ya kiafya ambayo huweza kusaidika kwa mti huu ni pamoja na matatizo ya pumu, kifua, malaria sugu, matatizo ya kinywa, baridi yabisi pamoja na vidonda.

Ili mti huu uweze kumsaidia mtu mwenye tatizo la kifua mathalani mtu huyo atahitajika kuchukua majiani yake na kuyachemssha na kisha kujifusha kwa mvuke wake huku akiwa amejifunika nguo nzito kama blanketi na mara baada ya hapo uweza kujihisi nafuu.

Lakini kwa wale wenye vidonda huhitajika kuchukua majiani ya mti huo na kuyakausha kisha waandae unga wake na kupaka katika kidonda husika.

Ili kupata ufafanuzi kuhusu matatizo mengine kama vile baridi yabisi, matatizo ya kinywa, malaria sugu na pumu unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua dkmandaitz@gmail.com

Lakini pia undani wa makala hizi unaweza kuupata kupitia kitabu cha TAMBUA kinachotarajia kuingia sokoni siku si nyingi kutoka sasa.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment