Tuesday, 26 September 2017

Faida 5 za unga wa mbegu wa parachichi kiafya

Habari za Jumanne ya leo msomaji wetu wa www.dkmandai.com napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika muendelezo wetu wa kufahamishana namna mimea na matunda yanavyoweza kuwa msaada mzuri katika afya zetu.

Leo tena nimekuja na hii faida nyingine ya parachicihi, lakini leo tiba itahusika zaidi katika matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la parachichi.

Kwanza mbegu ya parachichi huweza kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants'  hii ni kutokana mbegu hiyo na kuwa na zaidi ya asilimia 70 ya kirutubisho hicho.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanyika mwaka 2004 chini ya chuo kikuu cha Singapore na kuchapishwa katika Food chemistry walibaini kuwa mbegu hiyo inakiwango kikubwa cha antioxidants ikiwa ni pamoja na mbegu za matunda mengine kama vile embe, stafeli n.k

Mbegu hii ya parachichi pia huweza kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito kwani matumizi ya mbegu hiyo husaidia kuunguza mafuta mwilini  na hivyo kupunguza uzito mkubwa mwilini.

Matumizi ya unga wa mbegu hizo pia husaidia kupunguza shida ya maumivu ya mwili hasa kwenye maungio yaani 'joint' za mwili.

Lakini pia kwa wenye shida ya maumivu ya viungo hivyo wanashauriwa kutumia hata mafuta ya parachichi yenyewe kwani huweza kutoa ahueni kwa haraka zaidi.

Pamoja na hayo pia mbegu za parachichi husaidia kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni.

Jinsi ya Kutumia
Saga mbegu ya parachichi kisha changanya na maji ya uvuguvugu kisha koroga vizuri na utumie mchanganyiko huo kutwa mara 2 kwa siku kwwa muda wa wiki 2 mfululizo


Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

2 comments:

  1. Asante kwa maelezo mazur Dr,naomba kujua kipimo cha maji na kiasi cha unga kama dose moja kila siku

    ReplyDelete
  2. Asante sana Mtaalam Dr. Mandai kwa Afya update naahidi kufanyia exercise.

    ReplyDelete