Wednesday, 27 September 2017

Juisi ya karoti inavyoweza kukuokoa kwenye matatizo haya 5

Karoti ni moja ya kiungo/ tunda ambalo wengi tunakifahamu na huwa tunatumia kwa kuweka kwenye baadhi ya vyakula kwa lengo la kuongeza ladha na mvuto wa rangi ya chakula.

Karoti imesheni virtubisho vingi na muhimu na madini ambavyo vyote kwa pamoja hutusaidia sana kutukinga na kutibu dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya uoni hafifu, ngozi, nywele na kucha n.k

Unywaji wa juisi ya karoti kila siku ni mzuri na ni vyema ukafanya hivyo kama unaweza hii ni kutokana na faida za juisi hiyo kiafya ambazo nitaziorodhesha hapa chini:-

Miongoni mwa faida za juisi ya karoti ni pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Pia juisi hii inasifika kwa kuongeza uoni mzuri kwa mtumiaji kwani husaidia sehemu ya ndani ya jicho (retina) kuwa vizuri zaidi kutokana na kuwa na virutubisho vya 'lutein'  na 'beta -carotene' .

Aidha, juisi hiyo pia husaidia kurekebisha kiwango cha sukari ndani ya mwili na kushusha kiwango cha cholesterol ndani ya mwili.

Pamoja na hayo,  juisi hii ni kwa kuboresha afya ya ngozi na huweza kutumika kumpunguzia mtumiaji uwezo wa kupata tatizo la saratani.

Unaweza kuwasiliana nasi zaidi kwa ushauri zaidi kuhusu lishe kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment