Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 5 September 2017

Ifahamu hii kazi ya mchanganyiko wa asali na kitunguu maji


Hivi umewahi kufikiri kuhusu matumizi ya aina yoyote ya mchanganyiko wa juisi ya kitunguu maji na asali? Kama umewahi kufikiri kuhusu hili je, ulihisi faida zake ni zipi?

Sasa leo naomba nikueleze msomaji wangu miongoni mwa faida za mchanganyiko huo hasa katika urembo hususani kwa kinadada wenye uhitaji wa kuwa na nywele zenye afya na zisizokatika hovyo.

Unachopaswa kufanya ni kupata vitunguu maji kadhaa pamoja na asali halisi, kisha katakata vitunguu vyako na uviweke kwenye blenda na usage na kupata juisi yake.

Baada ya kupata juisi hiyo ongeza vijiko vya asali vitatu au viwili vya chakula na uchanganye vizuri  pamoja na juisi ya kitunguu.

Tumia mchanganyiko huo kupaka kwenye nywele zako na uhakikishe umegusa hadi kwenye shina la nywele zako kisha acha mchanganyiko huu kwa mda wa nusu saa kabla ya kuosha kichwa au kama ni usiku unaweza kulala hivyo hivyo na kuosha asubuhi.

Fanya zoezi hili ndani ya mwezi mmoja na utaona mabadiliko katika nywele zako kwani hazitakatika hovyo na zitakuwa na afya nzuri na hazitakuwa na mba pia.

Kwa ushauri zaidi kuhusu mada hii au mambo mengine hasa yanayohusu lishe bora unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment