Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 4 September 2017

Ifahamu hii njia asili ya kuponya matatizo ya fizi

Inawezekana ukawa ni miongoni kati ya watu ambao huwa unasumbuliwa na tatizo la fizi kutoka damu mara kwa mara na hujajua nini cha kufanya ili kumaliza tatizo hilo.

Matatizo ya fizi pia huweza kuchangia meno kutokuwa imara na kung'oka kirahisi zaidi, hivyo unapokuwa na tatizo hili la fizi huweza kuchangia na matatizo ya meno kwa ujumla.

Hivyo kama wewe ni miongoni kati ya watu ambao husumbuliwa na tatizo la fizi kuuma au kutoa damu, napenda kukwambia kuwa unaweza kutumia aloe vera kumaliza shida hiyo.

Unachohitajika kufanya ni kupata kipande cha aloe vera kisha sugua kwenye fizi zako au unaweza kausha majani ya alovera kisha saga na utumie unga wake kuweka kwenye mswaki wako na kupigia kama dawa. Kufanya hivyo pia husaidia kuponya vidonda vya mdomoni kama vipo na maambukizi mbalimbali.

Unaweza fanya zoezi hilo mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni kwa siku tano mfululizo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment