Wednesday, 20 September 2017

Jinsi nanasi linavyoweza kukuokoa kama unashida ya figo

kidney-stone,-pineapple
Nanasi ni moja ya tunda ambalo hupendwa na watu wengi ulimwenguni si kwasababu ya kutambua faida zake, lakini ni kutokana na kuwa na ladha nzuri pia.

Matumizi ya juisi halisi ya nanasi huenda yakawa na faida pia katika miili yetu kutokana na kuwa na virutubisho kadhaa ambavyo ni muhimu mwilini pia.

Miongoni mwa faida za kunywa juisi halisi ya nanasi ni pamoja na kusaidia mmen’genyo wa chakula kuwa katika hali nzuri, lakini zaidi juisi hii huweza kutoa ahueni kwa wenye shida ya mawe kwenye figo.

Juisi hii ina kiwango hafifu cha madini ya 'potassium' hali inayopelekea juisi hiyo kuwa rafiki kwa watu wenye matatizo sugu ya figo. Ili kunafaika na kinywaji hiki utapaswa angalau kunywa glasi moja hadi mbili za juisi ya nanasi kila siku kwa miezi kadhaa mfululizo.

Mbali na uwezo huo wa juisi ya nanasi, lakini pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kupunguza sumu mwilini hasa pale figo inapokuwa imeanza kuathirika na matatizo kadhaa.

Miongoni mwa njia nyingine zinazoweza kukusaidia kusafisha figo zako ni pamoja na kunywa maji ya kutosha kila siku ambayo hupelekea kupata haja ndogo (mkojo) kila mara na hivyo kusafisha mwili pia.

Kwa ushauri zaidi kuhusu lishe na ulaji wa vyakula na matunda kwa ujumla unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment