Tuesday, 26 September 2017

Kazi nyingine ya ukwaju itakayokushangaza mwanamke


Ukwaju wengi tumekuwa tukiufahamu na hasa umekuwa ukitumika katika kutengenezea juisi ambayo huwa na ladha ya uchachu na kuambata na faida kadhaa kwa mtumiaji wa juisi hiyo.

Lakini mbali na tunda hilo kuweza kutumika katika kuandalia juisi napenda kukufahamisha msomaji wangu kwamba unaweza kutumia tunda hili kwa kuboresha urembo wango hasa katika nyanja ya urembo wa nywele.

Ikiwa unasumbuliwa na tatizo la nywele zako kukatika hovyo mara kwa mara na kuzifanya kutokukua vyema basi unaweza kujaribu ukwaju.

Jinsi ya Kufanya
Chukua ukwaju kiasi na uuchemshe kwenye maji kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kisha acha ipoe na baadaye tumia maji hayo kuoshea kichwa chako, lakini hakikisha maji hayo yanafika kwenye shina kabisa la nywele zako.

Baada ya hapo kaa bila kunawa kwa muda wa saa 1 kisha osha kichwa chako. Fanya zoezi hili kila siku ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment