Tuesday, 26 September 2017

Kungumanga tunda lisilofahamika sana lakini linafaida lukukiKungumanga ni tunda linalopatikana kwa wingi katika bara la Asia, Idia pamoja na nchi za falme za kiarabu.

Kwa hapa nchini matunda haya yamekuwa yakipatikana zaidi kwenye baadhi ya maduka ya dawa za asili.

Tunda hili, licha ya kutofahamika sana miongoni mwa watu wengi, lakini limesheheni faida kadhaa kwa watumiaji.

Miongoni mwa faida za tunda hili ni pamoja na kusafisha kibofu cha mkojo sambamba na kuboresha afya ya figo.

Aidha, tunda hili husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini kwani husaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa kongosho mwilini.

Pia baadhi ya wanawake wenye changamoto ya maumivu wakati wa hedhi wanaweza kutumia kungu manga kumaliza hali hiyo.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua kungu manga na utengeneze unga wake halafu changanya na maji ya moto kwenye glasi kisha tumia hivyo kila siku asubuhi na jioni ndani ya siku 14.

Hayo ni machache lakini kwa mengi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment