Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 14 September 2017

Kula samaki angalau kwa wiki mara 2 upate faida hizi

Samaki wanasifika kwa kuwa na virutubisho ambavyo humuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka pamoja na virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na saratani mwilini.


Hali kadhalika, ulaji wa samaki pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini, hivyo kumsaidia mhusika kuepuka hatari ya kukumbwa na matatizo ya moyo.


Pia matumizi ya samaki huweza kumsaidia mhusika kutokumbwa na matatizo ya mwili kuvimba.


Huweza kupunguza uwezekano wa shinikizo la damu kutokana na kuwa na virutubisho ambavyo husaidia kuboresha afya ya moyo kutokana na kuwa na omega 3 ndani yake.


Aidha, unapotumia samaki husaidia kumpatia mlaji virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na protini, vitamini B3, vitamin D, vitamini B6, Omega 3 Fatty Acids. nk


Pamoja na hayo, matumizi ya samaki pia husaidia kuongeza uwezo wa kumbukumbu na hivyo kuondokana na tatizo la kusahau sahau.

Kwa ushauri zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment