Wednesday, 20 September 2017

Mambo ya msingi unayopaswa kuyajua kuhusu pilipili manga

Benefits Of Black Pepper
Viungo  vya vyakula mbalimbali mara nyingi kazi yake kubwa huwa ni kubadili rangi ya chakula na kuongeza ladha ya chakula.

Hata hivyo, viungo hivi vinasifika pia kwa kuwa na manufaa kadhaa kwa miili yetu.

Leo naomba kukueleza kuhusu faida za pilipili manga kwa afya zetu

Miongoni mwa faida za kiungo hiki ni pamoja na kupunguza maumivu ya viungo na kupunguza kiwango cha gesi tumboni.

Pia kiungo hiki husaidia kuboresha mfumo mzima wa tumbo mwilini na kupunguza kiwango cha tindikali mwilini.

Pamoja na hayo, kiungo hiki hupunguza uwezekano wa shinikizo la damu na kutoa kinga dhidi ya saratani kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants'.

Mbali na hayo, kiungo hiki pia husaidia kuzuia meno kuharibika na kulinda afya ya ngozi, nywele hususani katika kuondoa tatizo la mba.

Kwa taarifa zaidi au maelezo zaidi kuhusu lishe bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com  

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment