Monday, 25 September 2017

Msaada wa binzari kwa afya zetu


Binzari ni kiungo kinachotokana na mmea unaofahamika kama manjano.

Hata hivyo, licha ya kuwa wapishi hupenda kuitumia binzari kama kiungo, lakini si wote wenye ufahamu kuwa kiungo hiki kinamanufaa kwa afya.

Iwapo watu wengi wangekuwa na ufahamu kuhusu kiungo hiki nadhani kwamba wapishi wengi au familia nyingi zisingeacha kutumia kiungo hiki.

Miongoni mwa faida za kiungo hiki ni pamoja na kusaidia kurekebisha mapigo ya moyo kwa wenye shida ya shinikizo la damu.

Faida nyingine ni pamoja na kusaidia kibofu cha mkojo kufanya kazi vizuri pamoja na kuimarisha afya ya figo.

Ili kiungo hiki kikusaidia unaweza kutumia gramu gramu 2 au 3 katika maziwa freshi au maji ya moto, tumia mchanganyiko huo kwa wiki 2 hadi mwezi hasa kwa wazee wenye changamoto ya matatizo kwenye njia ya haja ndogo.

Hayo ni machache kuhusu binzari, lakini kwa undani zaidi kuhusu kiungo hiki usikose kujipatia kitabu cha 'TAMBUA' vol 2 kitakacho kujia hivi karibuni

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment