Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 2 September 2017

Njia 2 asili za kuzuia kutokwa na jasho sana 'sweating'


Habari za Jumamosi ya Septemba 2, 2017 mpendwa msomaji wangu wa www.dkmandai.com, leo napenda tuzungumze kuhusu tatizo la kutokwa na jasho kupita kiasi.

Kwanza ni vizuri ikafahamika kwamba kutokwa jasho ni njia mojawapo ya mwili kutoa taka, lakini pia ni mfumo unaotumiwa na mwili ili kuupooza pale hali ya hewa au joto la mwili linapokuwa limepanda.

Kila mtu huweza kutokwa na jasho, lakini kwa kawaida mwili hutoa jasho baada ya mtu kufanya shughuli fulani ya kufanya joto la mwili kupanda, lakini pia jasho huweza kutoka endapo mhusika atakumbwa na msisimko fulani, basi hapo pia jasho linaweza kumtoka.

Aidha, kuna baadhi ya watu ambao mbali na sababu hizo hapo juu, huweza kujikuta wakitokwa na jasho licha ya kuwa hawajafanya shughuli yoyote wala hawajakumbwa na msisimko wa aina yoyote ile na kitaalam tatizo hilo hufahamika kama 'hyperhidrosis.'

Moja ya mambo ambayo huweza kusaidia kuondoa tatizo hili ni pamoja na unywaji wa juisi ya nyanya endapo itaandaliwa vyema. Juisi hii inavitamin mbalimbali pamoja na madini ya 'potassium' sambamba na vitamin C.

Pamoja na hayo, kiazi mviringo pia huweza kutatua changamoto ya tatizo hili la kutokwa na jasho kupita kiasi, namna ya kufanya ni kukata vipande vya viazi hivyo kisha kusugua taratibu sehemu ambazo hutoa jasho kama vile kwapani. Zoezi hili likifanyika mara kwa mara huweza kuzuia tatizo hilo.
Kumbuka kuwa pia tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment