Saturday, 30 September 2017

Njia 6 rahisi za kupambana na mambo ya kuhuzunisha katika maisha


Maisha yetu binadamu huwa na panda shuka nyingi za hapa na pale ambazo nyingine huweza kutukatisha tamaa kabisa na kushindwa hata kuishi kwa amani kabisa.

Najua huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao kuna wakati unapitia changamoto za kimaisha hadi kupelekea kukata tamaa kabisa.

Leo niomba kukwambia haya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuhuzunisha katika maisha yako na hta kukukatisha tamaa ya kuishi kabisa, lakini pia nitakupatia na namna ya kuyakabili mambo hayo pindi yanapotokea.

1. Kuondokewa na mtu muhimu katika maisha (kufiwa)
Inapotokea mtu unayempenda akafariki ghafla hii huwza kuchangia hali ya huzuni sana kwako, inaweza kuwa kifo cha mzazi, mtoto au mke/ mme.

Hali hiyo mara nyingi huchangia msongo wa mawazo kwa wahusika wanaobaki hasa wale wakaribu zaidi , lakini pamoja na hayo lazima maisha yaendelee na unaweza kufanya haya ili kusahau tukio hilo na kusonga mbele kimaisha.

Kwanza ni kukubaliana na hali hiyo kuwa huenda mume / mke amefariki na kujua kuwa hawezi kurudi hata iweje na hata ukiendelea kulia haitasaidia chochote.

Jambo jingine nikuepuka kukaa pekee yako muda mwingi na kuepuka kutazama picha zake au kwenda makaburini bila kuwa na sababu za msingi.

Pia jaribu kukaa karibu na watu unaowapenda na kuepuka kuvuta taswira ya maisha mliyokuwa mkiishi pamoja na upuke kuzungumzia habari zake na ikibidi hama chumba mlichokuwa mkilala wote wakati ukifika tafuta mwenza mpya.

2. Kuachana /talaka
Kuachana ni moja ya mambo ambayo pia huwahuzunisha wahusika, lakini wengi ambao hukubwa na kadhia hii ni wanawake zaidi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba wanaoumia zaidi kutokana na talaka au kuachana ni wale ambao huachana bila uwepo wa sababu za msingi.

Mwanamke au mwanaume alitetalakiwa huweza kukumbwa na msongo wa mawazo, hasa pale anapozifikiria sababu zisizo na msingi za kuachwa au kuachana.

Hali ya msongo wa mawazo inapozidi sana huweza kuchangia matatizo kadhaa ya kiafya  hasa magonjwa yasiyoambukiza, hivyo ni vyema kukabiliana na hali hii kwa kutambua kuwa jambo la kuachana si kashfa kwako, hivyo inapotokea mkaachana lazima utambue kuwa unahitajika kujiamini na kuongeza jitihada za kuishi vizuri zaidi katika jamii inayokuzunguka ili kuiaminisha jamii yako kuwa mhusika hakustahili kukuacha.

Inapotekea mmeachana inakupasa utenge muda mwingi kwaajili ya kufanya kazi zako au biashara zako kwa bidii zaidia ili kudhibitisha uwezo wako wa kuishi na kufanikiwa hata kama upo pekee yako.

Epuka kupanga kulipa visasi  na acha kabisa kufuatilia mienendo yake tena na ikibidi jitahidi kuepuka kuwasiliana naye tena mara kwa mara

3. Kufukuzwa kazi
Wengi huchanganyikiwa mara tunapofukuzwa kazi kwani akili hutafsiri kuwa maisha yanakwenda mwisho hususani katika kushindwa kutimiza majukumu ya kifamilia, hii hutokana na vyanzo vya mapato kukoma.

Mara nyingi mtu unapokuwa na kazi heshima katika jamii huwa juu, lakini unapokuwa hauna kazi hata heshima huweza kushuka kuanzia ngazi ya familia hadi katika jamii pia, hivyo hali hiyo huwafanya watu wengi kuingia kwenye dibwi la msongo mkubwa wa mawazo na kuharibu zaidi afya zao.

Ni vyema kutojifungia ndani na kuwaza muda wote pale unapofukuzwa kazi, unachopaswa kufanya kwa wakati huo ni kuzingatia kukitumia vizuri kidogo ulichonacho kwa wakati huo na kupunguza kiwango cha matumizi yako ya kila siku, huku ukiendelea kutafuta kazi mpya kwa wale unaofahamiana nao.

Pia kipindi hiki unaweza kuomba msaada kwa ndugu wa karibu, lakini si kila ndugu kwani si vyema pia kutangaza shida zako kwa kila mtu.

Ili kupunguza msongo wa mawazo unaweza kutenga muda wa kusikiliza aina ya muziki unaoupenda na kama utakuwa ulipewa mafao yako baada ya tukio la kufukuzwa kazi basi unaweza kuyatumia kwa umakini kwa kutafakari biashara rahisi ya kuanza nayo.

5. Kushika mimba
Hali ya mwanamke kuwa mjamzito huweza kuchangia hofu kwa baadhi ya wanawake ikiwa ni pamoja na hofu ya kujifungua salama.

Hofu hiyo huweza kuzuiwa kwa mama mjamzito kukaa karibu na watu na kupata ushauri mzuri kutoka kwa wataalam wa afya pamoja na kufanya mazoezi.

Kipindi hiki mama mjamzito anatakiwa kuepuka kusikiliza habari za kuhusu matukio ya vifo vya wanawake waliopoteza maisha wakati wa kujifungua kwani huchangia kuongeza hofu zaidi kwa wanawake wajawazito.

Pia kipindi hiki ili mama abaki na afya bora na ajifungue salama huhitaji ukaribu wa kipekee, kuangalia sinema za kufurahisha na kusikiliza nyimbo nzuri na endapo mama atakuwa na dalili ambazo si nzuri ni vyema kumfikisha kwenye kituo cha afya kuliko kumtisha.

6. Matatizo katika tendo la ndoa
Wanaume wenye shida ya upungufu wa nguvu za kiume, huweza kukosa raha katika maisha na kuishi na msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa vilivyo, hali hii pia huweza kutokea hata kwa wanawake wenye shida ya kukosa hamu ya tendo hilo au kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Inashauriwa kuepuka msongo wa mawazo kuhusu tatizo hili na badala yake tumia muda kuangalia ni sehemu gani inaweza kukusaidia kumaliza shida hiyo kwa taratibu bila kukurupuka.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment