Tuesday, 19 September 2017

Sababu 5 zinazoweza kukufanya uzeeke mapema

Watu wengi miaka ya hivi karibuni wamekuwa wanaogopa sana uzee na wengine wamejikuta hata wakikanusha kuwa wao si wazee hata pale wanapoonekana tayari wameanza kuzeeka.


Leo ninazo hizi sababu ambazo zinaweza kukufanya muonekano wako uonekane umezeeka hata kama umri wako bado au kuzeeka kwa haraka zaidi.


Kutofanya mazoezi

Mazoezi ni muhimu sana kwa mtu mtu yoyote kwani husaidia ngozi ya mwili kuendelea kuwa vizuri. Hivyo ni vizuri kufanya mazoezi angalau dakika 20 kwa siku.


Kukosa usingizi.
Kwa kawaida binadamu anatakiwa apate muda wa kulala angalau saa 7 hadi 8 siku haijalishi yuko.


Uvutaji wa sigara
Sigara si nzuri kiafya na huchangia kuuchosha mwili mapema hivyo ni vyema kama unatumia sigara ukaacha mara moja na kama unashindwa unaweza kuwatafuta wataalam wakusaidie.


Acha kubeba visasi moyoni
Jifunze kusamehe watu ambao wamekukosea maishani, kwani unaposamehe unaufanya moyo wako kuwa safi. Watu ambao wanabeba visasi na vinyongo hupata makunyazi ya ngozi na kuzeeka haraka.


Kunywa pombe sana
Watumiaji wa vileo kwa wingi huwa katika hatari pia ya kuzeeka mapema

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment