Friday, 22 September 2017

Sababu za kupatwa na vidonda vya koo & namna ya kuvikabili

Kuna wakati unaweza kujikuta unasumbuliwa na maumivu ya koo au kupata vidonda vya kwenye koo na hivyo kukupa wakati mgumu hasa wakati wa kumeza vyakula, lakini usijue nini sababu.
Zipo sababu kadhaa zinazoweza kusababisha mtu kupatwa na vidonda kooni ikiwa ni pamoja na maambukizi ya bakteria au sababu nyingine za kimazingira na mzio (allergy) fulanifulani.

Pia vidonda hivyo pia kuna wakati huweza kuashiria dalili za maambukizi ya HIV au saratani ya koo. 

Njia ambazo huweza kumaliza shida ya maumivu ya kooni ni pamoja na hizi zifuatazo.

1. Ukwaju
Unachopaswa kufanya ni kuandaa juisi ya ukwaju kisha kunywa glasi moja ya juisi hiyo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja .

2. Kitunguu swaumu
Kama pia unapata shida wakati wa kumeza chakula kwaajili ya vidonda kwenye koo basi pia tambua unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa mafuta yake ambapo mhusika atatumia mafuta hayao kiasi cha matonoe manne au matano na kuchanganya na maji kiasi cha ribo kikombe cha chai na kunywa maji hayo kila siku ndani ya wiki 2.

3. Mbegu za uwatu
Chukua mbegu hizo za uwatu kiasi cha vijiko viwili vya chakula halafu weka kwenye maji kiasi cha glasi mbili kisha weka kwenye sufuria na uchemshe hadi zichemke vizuri halafu yaache maji hayo yapoe kiasi kisha chuja na unywe maji hayo kwa siku mara mbili asubuhi na jioni kwa siku 5.

4. Mdalasini & asali

Chukua mafuta ya mdalasini kiasi cha matone matatu halafu changanya na asali kijiko kimoja cha chai kisha tumia mchanganyiko huo mara 3 kwa siku na itakusaidia.

Kwa ushauri zaidi kuhusu virtubisho asili kutoka kwetu unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment