Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 16 September 2017

Sababu za macho kuwa mekundu & njia za kumaliza tatizo hilo


Habari za leo mdau wangu wa tovuti hii naamini utakuwa upo vizuri, leo nimeona tufahamishane baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia wewe mwenye tatizo la mcho yako kuwa mekundu.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yakizingatiwa husaidia kuboresha afya ya macho.

1. Kutozingatia ulaji wa matunda na mboga za majani
Mbogamboga na matunda zinapokosekana mwilini mwako huweza kuwa chanzo cha tatizo  la macho kuwa na rangi mbaya kwani mboga hizo huwa na vitamin muhimu kwa ajili ya macho mfano A,C, na E ambazo kimsingi ndio muhimu sana kwa ajili ya macho.

2. Kutokupata muda wa kutosha wa kulala
Wataalam wa masuala ya afya wanaeleza kuwa kutopata muda wa kulala wa kutosha huweza kuwa sababu, hivyo wataalam hao hupendekeza binadamu alale angalau saa saba hadi nane kwa siku ili kuurudisha mwili uliochoka katika hali yake ya kawaida kwani mtu anayekosa usingizi wa kutosha ni rahisi kwake kuwa na macho mekundu kwa sababu ya uchovu.

3. Unywaji hafifu wa wa maji
Kutokunywa angalau glass 8 mpaka kumi kwa siku huweza kuchangia kuwa na macho yenye rangi ya hovyo, hivyo ni muhimu kwa afya ya macho yako kunywa maji mengi ambayo huenda kusafisha mwili wote na kuondoa sumu mwilini. kutokunywa maji huweza kuchangia mwili kuwa mkavu na macho mekundu.

4. Unatumia muda mwingi kufanya kazi za macho

Hii ni kwa wale ambao hufanya kazi ya computer au kuangalia movie hali hiyo nayo huchangia kuchosha macho na hivyo kuweza kuchangia kuwa mekundu.

5. Huenda unatumia pombe kupita kiasi

6. Huenda unakaa mazingira yenye vumbi na moshi


Zingatia
Ni vyema kuwaona wataalam wa macho ikiwa unaona tatizo hilo limeendelea kukusumbua kwa muda mrefu, lakini pia jenga utaratibu wa kuchunguza macho yako angalau mara mbili kwa mwaka kama wataalam wanavyoshauri.

Tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment