Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 4 September 2017

Ukiona dalili hizi 6 huenda utakuwa na shida kwenye mapafu yako

Mapafu ni miongoni mwa kati ya viungo muhimu ndani ya mwili ambavyo hufanya kazi kubwa ya kuhakikisha viungo vingine mwilini vinakuwa katika hali njema, kwani hufanya kazi kila wakati unapopumua.

Wakati unapopumua mapafu yako huchukua hewa ya 'oxygen' na kuiunganisha pamoja na mzunguko wa damu mwilini kisha kusambaza sehemu mbalimbali za mwili, huku wakati huo huo mapafu hayo yakitoa hewa chafu ndani ya mwili inayofahamika kama 'carbon dioxide'

Hivyo kutokana na umuhimu huo wa mapafu kuna kila sababu za kila mtu kufahamu ishara zozote zitakazoainisha kuwa huenda kuna shida kwenye mapafu yake.

Miongoni mwa dalili mbaya kwa afya ya mapafu ni pamoja na hizi zifuatazo:-

1. Kikohozo kinachoendelea kwa muda mrefu licha ya matumizi ya dawa

2. Kupata taabu wakati wa upumuaji

3. Kuhisi kasauti fulani kamlio wakati wa upumuaji

4. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara hasa asubuhi

5. Kuhisi hali ya uchovu 

6. Kupata usingizi kwa tabu

Jinsi ya kufanya ili kuwa na mapafu yenye afya bora

1. Kuacha kuvuta sigara

2. Kuepuka kukaa/ kuishi na mtumiaji wa sigara

3. Epuka kuishi karibu na maeneo yenye msongamano wa viwanda

4. Panda mimea eneo lako la makazi ili kuboresha ubora wa hewa katika eneo lako n.k

Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandatz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment