Friday, 22 September 2017

Unga wa komamanga unaweza kukusaidia kama unatatizo la uzazi mwanamke


Ugumba kwa wanawake ni ile hali ya kushindwa kushika ujauzito kwa angalau mwaka mmoja wakati mwanamke husika akiendelea kukutana na mwenzi wake (tendo la ndoa) pasipo kinga yoyote.

Shirika la afya duniani linaeleza kuwa ugumba hujumuisha ile hali ya mwanamke kushika ujauzito na kushindwa kukaa nao hadi hatu ya mwisho ya kujifungua salama.

Tatizo hili la ugumba kwa wanawake huweza kuchangiwa na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na uvimbe kwenye kizazi, magonjwa ya zinaa, upungufu wa damu mwilini (anemia), kuziba kwa mirija ya uzazi pamoja na fangasi sehemu za siri.

Sababu nyingine za tatizo hili ni unywaji wa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara, uzito mkubwa, msongo wa mawazo, historia ya maumivu wakati wa hedhi, mlo kutokuwa bora na msongo wa mawazo.

Leo ninazo baadhi ya vyakula au matunda ambayo huweza kutoa ahueni kwa mwanamke mwenye shida ya uzazi (ugumba).

Komamanga
Tunga hili huweza kuhamasisha uzazi kwa wanawake wagumba, kwasababu husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenye mji wa uzazi na kusaidia kuzuia uwezekano wa mimba kutotoka.

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015 uliochapishwa kwenye jarida la 'pharmacognosy' ambalo hushughulika na madwa yatokanayo na mimea au vyanzo vingine vya asili walieleza kuwa mkomamanga unaweza kutumika kama kirutubisho cha kuongeza urefu wa kipindi cha uzazi kwa wanawake.

Kinachotumika katika tunda hilo ni mbegu zake zilizosagwa  na magome  kisha hutunzwa kwenye chombo kisichopitisha hewa. Kisha mchanganyiko huo unaweza kutumika kwa kuchanganywa na maji ya uvuguvugu na kunywa kila siku kwa muda wa wiki kadhaa.

Kama utahitaji kupata ufafanuzi wa kina zaidi kuhusu maandalizi ya mchanganyiko huo ili uweze kukusaidia basi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege ulizia kwa Mtaalam Mandai.


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment