Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 11 September 2017

Virutubisho muhimu vinavyohitajika kwa mwanaume


Kuna baadhi ya virutubisho fulani huweza kuwa na umuhimu zaidi kwa jinsia fulani kutokana na aina ya maumbile ya jinsia husika.

Kwa kawaida vykula huusaidia mwili kupata vitamni mbalimbali na madini kadhaa ambayo huwa na faida zake ndani ya mwili.

Leo naomba nikueleze msomaji wangu baadhi ya vitamin ambazo huweza kuwa na umuhimu zaidi kwa jinsia ya kiume (wanaume)

1. Vitamin D
Hii ni vitamin muhimu kwa wanaume kutokana na kusaidia watu wa jinsia hiyo kuwa na mifupa imara, kulinda afya ya akili, kuzuia matatizo ya kihisia hususani unyogovu 'depression' na kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya 'testosteron' pamoja na kupunguza madhara ya matatizo ya maumivu ya viungo.

Unavyoweza kuipata Vitamin D
Vitamin D inapatikana kupitia ulaji wa mayai, uyoga, lakini pia huweza kupatikana kwa urahisi zaidi kupitia uotaji wa jua hasa lile la asubuhi.


2. Vitamin K
Ni vitamin muhumu pia kwani husaidia kumkinga mhusika dhidi ya matatizo ya moyo na huwasaidia wale wanaotumia dawa kali kwa kipindi kirefu kupunguza madhara ya dawa hizo mwilini.

Jinsi ya kuipata vitamin K
Hupatikana kwenye mboga za kijani  za majani, kabeji, broccol n.k

3. Magnesium 
Madini haya nayo ni muhimu mwilini mwa mwanaume kwani husaidia kumkinda mhusika dhidi ya matatizo ya presha, misuli na kuboresha mbegu za kiume (manii)

Madini haya hupatikana zaidi kupitia mboga za majani, bidhaa za baharini na karanga

4. Potassium
Ni muhimu pia kwani husaidia shinikizo la damu la kupanda, huboresha afya ya mifupa na kupunguza hali ya uchovu,.

Pia husaidia kuboresha mbegu za kiume na kuboresha afya ya misuli na kupunguza madhara ya kisukari.

Madini haya huweza kupatikana kupitia ndizi, viazi vitamu, maharage, parachichi


Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kumpigia simu Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment