Thursday, 28 September 2017

Vyakula kwa wenye vidonda vya tumbo vyenye uwezo wa kuondoa madhara


Mara nyingi watu wenye kusumbuliwa vidonda vya tumbo hupelekea kubadili mpangilio wa mlo na ratiba nzima ya upataji wa milo hiyo.

Zoezi hilo la kubadili mpangilio na ratiba ya mlo hufanyika kwa lengo la kutoa ahueni kwa mgonjwa husika na kupunguza madhara ya tatizo hilo.

Yafuatayo ni mambo ambayo mtu mwenye vidonda vya tumbo anaweza kutumia wakati wa tatizo hilo.

1. Kupata mlo mdogo, lakini mara kwa mara ili kupunguza mzigo mzito kwa mfumo wa umeng'enyaji chakula na hivyo kupunguza madhara ya tatizo hilo.

2. Kula vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi zaidi, ongezeko la aina hii ya chakula husaidia kurejesha sehemu zilizoathirika na kupunguza zaidi madhara ya tatizo.

3. Kula zaidi mboga za majani, ulaji wa mboga hizi mara kwa mara husaidia kuongeza vitamin K mwilini, ambayo husaidia kurejesha sehemu za tumbo zilizoathirika au kuharibika.

4. Juisi ya kabeji, juisi hii hufaa kwa watu wenye vidonda vya tumbo kutokana na kuwa na uwezo wa kuponya matatizo ya vidonda vya tumbo.

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment