Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 12 September 2017

Vyakula & vinywaji usivyotakiwa kutumia kama unahitaji kupunguza kitambiZOEZI la kupunguza uzito si jambo jepesi sana kwani linahitaji umakini sana hususani katika mtindo wa maisha na hata mabadiliko ya ratiba ya mlo.

Leo napenda kukufahamisha hii orodha fupi ya vyakula ambavyo hupaswi kuvitumia wakati ukiwa katika harakati za kupunguza mwili au uzito

Vitu vyenye mafuta mengi hii ni kwasababu chakula hicho kimesheheni 'calories' na 'fat' ambayo huweza kuchangia mwili kuendelea kunenepa, lakini pia chakula hicho huongeza kiwango cha sukari kwenye damu na hivyo kuchangia mhusika kushindwa kufanikiwa kupunguza mwili.

Mtaumizi ya soda, ikiwa unahitaji kupunguza mwili pia ni muhimu kuepuka matumizi ya vinjwaji baridi hususani soda.

Kwa mujibu wa utafiti ulifanyika mwaka 2015 na kuchapishwa kwenye jarida la American Geriatrics Society walibaini kuwa watu wanaokunyw soda mara tatu kwa siku huweza kuongezeka unene zaidi ya miaka 9 kuliko wale ambao hawakunywa soda.

Bisi au Popcorn 
Bisi ni kitafunwa kizuri na huburudisha kinywa, lakini pia kitafunwa hiki hakiwezi kumfaa mtu mwenye malengo ya kupunguza mwili kwasababu kimesheheni 'carbohydrates' ambayo husaidia kuongeza nguvu mwilini na hivyo kuongeza mwili pia ikiwa kiburudisho hicho kitatumika mara kwa mara.

Matumizi ya mkate mweupe 'White bread'
Mkate una kiwango kikubwa cha 'carbohydrates' ambacho nacho huweza kufifisha juhudi zako za kupunguza mwili.

Matumizi ya bia
Kama kweli unatamani kupungua uzito ni vyema pia ukaacha kutumia bia

Kwa ushauri zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment