Wednesday, 27 September 2017

Zabibu tunda lenye nafasi ya kuwasaidia wenye pumu


Zabibu ni matunda ambayo huwa na rangi nyekundu , nyeusi na baadhi huweza kuwa na rangi ya kijani , njano na hata pinki pia, lakini kwa hapa Tanzania tumezoea yale ya rangi nyeusi.

Mtaalam wa tiba lishe, Abdallah Mandai anasema kuwa zabibu ni miongoni mwa matunda yenye faida kwa afya ya mwanadamu ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya ya mishipa ya damu, hivyo kupunguza nafasi ya kuibuka kwa hatari ya magonjwa ya moyo pamoja na saratani.

Zabibu pia inasifika kwa uwezo wake wa kuongeza damu mwilini pale zinapotumiwa mara kwa mara.

Ulaji wa zabibu pia husaidia kumaliza tatizo la ukosefu wa haja kubwa, kwani ndani yake kuna asili ya nyuzinyuzi ambazo ni muhimu katika umeng’enyaji chakula na kumsaidia mhusika kupata choo kwa urahisi zaidi.

Aidha, matunda haya husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari ya asili huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.

Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Zabibu pia husaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza uwezekano wa mhusika au mtumiaji wa matunda haya kukumbwa na matatizo ya hewa hususani pumu.

Kichana cha zabibu

Mvinyo utokanao na zabibu husaidia kuongeza bacteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo (normal flora) kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo kuwa rahisi.

Ndani ya zabibu kuna virutubisho mchanganyiko kama vile 'copper' , madini chuma na 'manganese', ambayo yote kwa pamoja ni muhimu kwa uimarishaji wa afya ya mifupa mwilini. Hivyo matumizi ya mara kwa mara ya matunda haya huweza kupunguza madhara ya maumivu ya mifupa kwa watu wenye umri mkubwa (wazee).

Kwa msaada zaidi kuhusu lishe bora au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment