Thursday, 21 September 2017

Zifahamu hizi kazi za mafuta ya nazi & aloe vera


Bila shaka utakuwa unafahamu kuhusu mafuta ya nazi , lakini pia huenda unafahamu kuhusu mmea wa aloe vera.

Pamoja na kuyafahamu hayo pia ningependa kuja kama utakuwa unafahamu kuhusu bawasiri ? Huu ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu hufahamika kama 'hemorrhoids' tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto.

Leo nimeona nikueleza msomaji wangu wa www.dkmandai.com jinsi tatizo hili linavyoweza kusaidika kwa kutumia mafuta ya nazi na aloe vera


1. Mafuta ya nazi
Mhusika atatakiwa kuyapata mafuta halisi kabisa ya nazi na si ya dukani kisha kupaka sehemu yenye tatizo kutwa mara mbili. Zoezi hilo lifanyike hadi pale mhusika atakapoona mabadiliko au kuisha kwa tatizo.


2. Aloe Vera
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta majani ya mualovera baada ya kuchuma ule utomvu wake utautumia kwa kupaka sehemu yenye tatizo kutwa mara tatu.


Zingatia
Njia zote hizo mbili huweza kutoa matokeo mazuri kutegemea na juhusdi za mtumiaji pia huweza kuwa kama kinga ya tatizo hilo.


Kama utakuwa na swali usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba  0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

1 comment: