Friday, 13 October 2017

Baadhi ya magonjwa ambayo dalili zake huanzia kwenye uchovu


Kila mtu huhitaji kuwa mwenye nguvu na mchangamfu kila siku ili kuweza kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali za kila siku.

Lakini tatizo linakuja pale ambapo kila siku utajikuta ukiamka ukiwa mchovu na usiyetamani kufanya chochote kabisa zaidi ya kukaa tu.

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa unapokumbwa na hali hiyo basi huwa kuna sababu na zifuatazo ni baadhi tu ya sababu ambazo huweza kumfanya mtu kuhisi uchovu.

Kisukari (Diabetes)
Kuhisi uchovu wa kila siku na mara kwa mara huweza kuwa ni kiashiria cha ugonjwa wa kisukari. Hivyo ikiwa unahisi hali hiyo kila siku na unapata haja ndogo mara kwa mara na uoni wako unakuwa hafifu basi unaweza kuonana na wataalam ili kufanya vipimo zaidi.

Pia kama unapata uchovu wa mara kwa mara huenda ikawa ni dalili ya matatizo ya moyo, hivyo ni nzuri ukaonana na wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Upungufu wa damu (Anemia)
Upungufu wa damu ni mojawapo ya chanzo cha mtu kuweza kuhisi hali ya uchovu wa mara kwa mara hususani kwa wanawake,

Ikiwa unapata muda mzuri wa kutosha na unapata virutubisho vyote muhimu na bado unapatwa na hali ya kuhisi uchovu basi ni vyema uende ukafanye uchunguzi kuona kama hauna tatizo la anemia.

Tatizo la upungufu wa damu mwilini ni rahisi sana kukabiliana nalo ambapo mgonjwa atatakiwa kupata virutubisho na vyakula vyenye madini chuma ndani yake.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment