Friday, 6 October 2017

Fahamu mpangilio mzuri wa mlo wako kiafya

Mpangilio wa chakula ni moja ya mambo muhimu kwa siha ya afya ya mwanadamu kutokana na vyakula kuwa na virutubisho mbalimbali.

Leo ninaye Mtaalam Mandai, ambaye anasema kuwa mbogamboga  na matunda ni muhimu sana kuwa katika ratiba ya mlo wako.

Pia mtaalam huyo anaendelea kueleza kuwa, ni vizuri kuwa na ratiba ya kula na kuzingatia suala la kubadilisha chakula chako kutoka mlo hadi mlo kwa kufuata ratiba utakayokuwa umeipanga, jambo la msingi ni kuhakikisha hauli aina nyingi ya vyakula katika mlo mmoja.

Aidha, Mtaalam Mandai anaongeza kuwa ni vyema kuwa na ratiba nzuri ya ulaji  kutokana na tabia hiyo kusaidia uyeyushaji wa chakula kwenda vizuri zaidi tofauti na yule ambaye anakula pasipo kuwa na ratiba maalum.

Pamoja na hayo, Mtaalam huyo anaongeza kuwa, unapozingatia kutumia vyakula vyenye nyuzi nyuzi pamoja na nafaka zisizokobolewa , humsaidia mhusika kuwa na afya bora hii ni kwa sababu vyakula vya aina hiyo ni bora zaidi kwa afya. Vyakula ambavyo hukobolewa sana huwa havifai sana kwa afya na hata pale mchele unapooshwa sana huweza kusababisha kuondoka kwa baadhi ya virutubisho muhimu.

Jambo jingine ambalo ni zuri kwa afya yako ni kuzingatia kula kile unachokipenda ili kustawisha afya na furaha yako, lakini zingatia kutokula kupita kiasi, kwani unapokula sana huweza kujikuta ukiwa mchomvu na kuzongwa na usingizi pamoja na kupunguza hata uwezo wa kufikiri.

Pia epuka matumizi ya vikolezo vyenye madhara, ambavyo ni pamoja na sukari, chumvi na mafuta ni vizuri ukahakikisha vitu hivyo unatumia kwa kiwango kidogo sana.

Hali kadhalika Mtaalam Mandai, anasema maji pia ni muhimu katika kukamirisha suala la mlo, hivyo ni vizuri ukanywa maji ya kutosha yaliyo safi na salama na inapendekezwa angalau glasi 8 hadi 10 kwa kutwa nzima, lakini zingatia usinywe maji wakati wa mlo au muda mfupi sana kabla ya kula. Muda sahihi wa kunywa maji ni dakika 30 kabla na baada ya kula hii husaidia myeyusho wa chakula kufanyika vizuri. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment